Ligi Kuu

‘Niliamini ni jaribio letu la mwisho..’-Fei Toto

Sambaza....

“ Lilikuwa ni jaribio zuri, niliona upenyo wakati nakwenda kupiga mpira ule na nilijua linaweza kuwa shuti letu la mwisho kupiga golini kwa KMC. Ilibidi nitulize akili yangu na namshukuru Mungu niliweza kupiga na mpira ulikwenda sahihi. Inasisimua kufunga goli la ushindi wakati kama ule lakini usisahau kuwa tulifanya kazi kama timu kwa dakika zote.” Anaanza kusema mfungaji wa goli la ushindi la Yanga SC dhidi ya KMC FC, Feisal Salum.

Kiungo huyo –namba sita alifunga goli kwa mkwaju wa faulo dakika ya 90’ ya mchezo na kuipa Yanga ushindi wa saba msimu huu katika ligi kuu Tanzania Bara. Yanga ilibanwa mno na ilikaribia kupoteza mechi kama si umahiri wa golikipa wao Beno Kakolanya lakini walipata alama tatu muhimu kwa msaada wa mpira wa faulo uliopigwa na Fei Toto dakika za mwisho za mchezo.

“ Muhimu tumeshinda mechi. Mapambano yanaendelea na sasa tunajiandaa na mchezo ujao dhidi ya Lipuli. Ilikuwa mechi ngumu lakini niwapongeze KMC pia walicheza vizuri na walikuwa wagumu sana katikati ya uwanja.”

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x