Sambaza....

Alexander Hleb huenda likawa sio jina pekee kuingia kichwani pindi unapokumbuka timu ya mwaka 2006 ya Arsenal ambayo ilikaribia kutwaa taji la kwanza la UEFA katika Historia ya klabu.

Lakini ilikuwa ndani ya Arsenal ambapo nyota huyo wa kimataifa wa Belarus alicheza kandanda safi katika maisha yake ya soka na hatimaye kupata uhamisho wa Pauni Milioni 12 kutua Barcelona majira ya kiangazi ya mwaka 2008.

Ungeweza kuhisi kwamba uhamisho wa ndotoni kwa mchezaji yoyote yule lakini kwake ilikuwa majanga makubwa, ambaye aliitumikia Barcelona mwaka mmoja kabla ya kuondoka kwa mkopo kwenda Stuttgart ya Ujerumani na hakurejea tena Hispania.

Image result for Alexander hleb images barcelona introduced day

 

” Ni bado ngumu kwangu kuelezea kwanini niliondoka Arsenal. Nilikuwa na furaha sana pale . Arsene Wenger aliniamini sana. Na halafu nikaamua kuondoka.”

“Nilikuwa likizo halafu mawakala na makocha walinishawishi kwamba nihamie Barcelona. Kiukweli nilikuwa sielewi nini nilikuwa nafanya. Ilifika muda nikashangaa ,” eeh Mungu naondoka Arsenal.”

“Pindi Arsene aliposema ni masaa tu yamebaki . nilijisikia vibaya , ilikuwa ngumu sana kukubali. Wenger alifanya kila awezalo kubaki na mimi Arsenal.”

“Na hata alinitumia ujumbe wa simu nilipokuwa navua samaki,” Alex, siwezi kukuachia, tunakuhitaji hapa , nililia nilipokuwa nasoma.”

 

Hleb amesema kwamba yeye ni mmoja wa wachezaji ambao wanajuta kuondoka Arsenal na kumuacha Wenger , lakini mahusiano yake na wenger bado ni mazuri.

 

” Wakati wa msimu wangu wa kwanza Uingereza, nilipata jeraha nilipokuwa nacheza timu ya taifa, kwahiyo nikawa nauguza jeraha ,nikamuambia Wenger kwamba italeta maana sana kama akinipeleka kwa mkopo Ujerumani au kokote kule.”

” Alikuwa kama,” Nyamaza! Nakuamini ! Usifikirie vitu kama hivyo tena ! Kiukweli ? nilipaa nje ya chumba , nilihisi kama nina mabawa.”

“Arsene anawependa sana wachezaji wake. Anasema kile ambacho mchezaji anataka kusikia . Nafikiri kuna wachezaji wachache sana ambao wanaweza kusema kwamba hawakufurahia kufanya nae kazi. Kila mtu alikuwa anaamini kwamba atapata nafasi. Na nafikiri wachezaji wengi walioondoka mwisho wa siku walijuta .”

Sambaza....