Mabingwa Ulaya

Rekodi zinavyompasua kichwa Pep Guardiola

Sambaza....

Ni mchezo wa robo fainali ya michuano Uefa Champions League, Liverpool dhidi ya Manchester City ni mchezo unaowakutanisha makocha bora kwa sasa barani Ulaya

Juggen Klopp ndiye kocha aliyefanikiwa kuwa kikwazo kwa Pep Guardiola, rekodi zinaonesha amemfunga mara sita katika michezo 12, waliyokutana ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko kocha yeyote Ulimwenguni

Rekodi hizi hapa


  • Borussia Dortmund 4-2 Bayern Munich (Germany Super cup, Julai 2013)
  • Borussia Dortmund 0-3 Bayern Munich (Bendesliga, Novemba 2013)
  • Bayern Munich 0-3 Borussia Dortmund (Bendesliga Aprili 2014)
  • Borussia Dortmund 0-2 Bayern Munich (Fainali ya Dfb Pokal, May 2014)
  • Borussia Dortmund 2-0 Bayern Munich (Dfl Super cup, Agosti 2014)
  • Bayern Munich 2-1 Borussia Dortmund (Bendesliga, Novemba 2014)
  • Borussia Dortmund 0-1 Bayern Munich (Bendesliga, Aprili 2015)
  • Bayern Munich 1-1 Borussia Dortmund (Dortmund wakashinda kwa penati 2-0 nusu fainali ya Dfb Pokal, Aprili 2015)
  • Liverpool 1-0 Manchester city (Ligi kuu ya Uingereza, Desemba 2016
  • Manchester city 1-1 Liverpool (Ligi kuu ya Uingereza, Machi 2017
  • Manchester city 5-0 Liverpool (Ligi kuu ya Uingereza Septemba 2017)
  • Liverpool 4-3 Manchester city (Ligi kuu ya Uingereza Januari 2018)

Anfield bado ni sehemu salama kwa Liverpool katika michuano ya Ulaya, katika michezo 14, ya hivi karibuni Liverpool haijapoteza wakiwa kunako uwanja wao huo mara ya mwisho kupoteza ilikuwa mwaka 2014 katika mchezo dhidi ya Real Madrid

Image result for liverpool vs manchester cityHii ni mara ya kwanza kwa Liverpool na Manchester City kukutana kunako michuano ya Ulaya, katika michezo 178 ya michuano tofauti ambapo Liverpool wameshinda michezo 87, wakifungwa 45, huku michezo 46, wakienda sare

Roberto Filminho ndiye mchezaji wa kuchungwa zaidi kwa upande wa Liverpool, hiyo ni kutokana na rekodi zake kunako michuano ya Uefa Champions League msimu huu akiwa ametupia kambani mabao 7, na assist 3 ambapo inafanya kuhusika katika upatikanaji wa mabao 10 mpaka sasa, hii ina maana ni Cristiano Ronaldo pekee ndiye anayemzidi katika rekodi hizi

Sergio Kun Aguero ndiye mchezaji tishio kwa safu ya ulinzi ya Liverpool mpaka sasa, katika michezo 18, waliyokutana mshambuliaji huyu amewafunga mara 6, pia akitoa usaidizi katika mabao matatu

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x