Blog

Rufaa ya Wambura imebeba mambo mazito

Sambaza....

Wakili wa Michael Richard Wambura, Emmanuel Muga amesema kuwa wameamua kukataa rufaa ili kutafuta haki yao, Wakili huyo amesema wameambatanisha mambo ya kisheria na mambo matano ya msingi yaliyopelekea kukata rufaa hiyo

“Tumeandaa rufaa na imekamilika, tumeshalipia kwa mujibu wa kanuni za TFF kuwa ilipiwe shilingi milioni moja, na kuanza taratibu za kuisajili ndani ya siku tatu kama tulivyoelekezwa

“Tumeambatanisha mambo mengi ya kisheria, na tumeeliezea mambo mengi ya msingi pia tupo tayari kwenda mbele ya kamati ya rufaa ya maadili kufafanua zaidi”

Aidha Wakili huyo alifafanua kuwa hukumu wameipata kwa njia ya tovuti ikiwa imechapwa na kuisikiliza, lakini kanuni haziwabani kuwa lazima waambatanishe wakati wa kukata rufaa, na wao wamekata rufaa kwa hati ya dharula ingawa haijawafikia rasmi

“Tumekata rufaa kwa hati ya dharula kwamba kamati ya rufaa ya maadili iitishwe haraka kusikiliza suala hili, kwa maana Wambura ana majukumu ya kitaifa na kimataifa itakumbukwa aliteuliwa kuwa kamishina wa mchezo utakaofanyika mwezi ujao wa U20 kati ya Kenya na Rwanda, hivyo lazima hatma yake ijulikane mapema

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x