Sambaza....

Kikosi cha Simbasc kinachofanya mazoezi yake katika uwanja wa BokkoBeach Veteran kinatarajiwa kuondoka mapema mwishoni mwa wiki tayari kuwakabili wapinzani wao Njombe Mji ya Njombe, mchezo utakaopigwa katika dimba la Sabasaba.

Kikosi cha Simba kitaondoka Jumamosi tarehe 31 asubuhi saa moja kwa njia ya barabara ili kuwahi Iringa kuzoea mazingira na hali ya hewa ambayo inatajwa kuwa na baridi kali. Huenda pia ikawajumuisha wachezaji wake waliokua majeruhi kwa muda mrefu Haruna Niyonzima na Salim Mbonde ambao wameungana na timu kufanya mazoezi kamili.

TareheMwenyeji-Mgeni

Mchezo huo awali ulikua uchezwe mapema mwezi huu lakini ulisogezwa mbele ili kupisha maandalizi ya Simba katika michuano ya Kimataifa. Hivyo mchezo huo umepangwa kupigwa April 3 mwaka huu.

Mara ya mwisho wawili hao kukutana timu ya Simba iliibuka na ushindi wa mabao manne kwa bila katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam.

Sambaza....