Sambaza....

Kikosi cha Simba sc kipo nchini Djibouti, tayari kwa mchezo wa marejeano wa michuano ya kombe la shrikidho dhidi ya wenyeji wao Gendermarie

Kikosi hicho, kilichoondoka mchana wa leo na kupitia Nairobi ambapo walilazimika kusubiri kwa muda mwingi na usiku huu kuwasili salama nchini Djibouti

Katika kile kilichooneka kikosi hicho kimejipanga kufanya vizuri kwenye mchezo huo, baada ya kufikia kunako Hotel ya kifahari iliyopo pembezoni mwa bahari hindi

Hotel hiyo ya Sheraton, ambayo ni moja ya hotel nchini humo ikitajwa kuwa na hadhi ya nyota 5

Simba sc, inataraji kushuka dimbani siku ya Jumanne kuumana na Gendermarie kwenye mchezo wa kombe la shirikisho la soka barani Afrika

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Simba ilipata ushindi wa mabao 4-0

Sambaza....