Sambaza....

Upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha wa dola za Kimarekani 375,418 inayomkabili raisi wa zamani wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Jamal Emily Malinzi, na wenzake umekamilika kunako Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Mwendesha mashitaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru, Leonard Swai, amemuelezea Hakimu Mkazi Kisutu Wilbard Mashauri kwamba upelelezi umekamilika

Image result for Malinzi

Aidha Swai, aliiomba Mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kusomewa maelezo ya awali kwa washitakiwa hao

Hakimu Mashauri amehairisha kesi hiyo, mpaka Aprili 11, 2018 ambapo washitakiwa hao watasomewa maelezo ya awali

Pamoja na Malinzi, washitawa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa na Nsiande Mwanga aliyekuwa Mhasibu wa TFF

Sambaza....