Sambaza....

MLINZI wa kati wa Kimataifa wa Togo, Vicent Bossou amesema yupo tayari kurejea Tanzania kucheza soka lakini kipaumbele chake kikubwa ni klabu yake ya zamani Yanga SC na Azam FC iliyo chini ya Mholland, Hans van der Pluijm.

Akizungumza na www.kandanda.co.tz akiwa Vietnam anakocheza hivi sasa mlinzi huyo mwenye uwezo wa kucheza pia nafasi ya mashambulizi amesema yupo huru kuzungumza na klabu yoyote kwa kuwa alisaini miezi sita tu katika klabu yake ya sasa.

” Kwa sasa naweza kupatikana, ni mchezaji huru kutokana na kusaini miezi sita tu nilipokuja huku.” anasema beki huyo mshindi wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili akiwa Yanga.

” Nipo tayari kurejea Tanzania, nawapenda mashabiki wa soka klatika nchi hiyo, ni watu wanaopenda mpira. nipo tayari kuchezea klabu yoyote tutakayoafikiana lakini kipaumbele changu kama nitarejea basi ningependa iwe Yanga au Azam FC.” anasema mchezaji huyo wa Togo na kuongeza

” Ikitokea, Simba kunihitaji hakuna tatizo, au klabu nyingine yoyte. ni suala la kukaa na kuzungumza kwa sababu hii ni kazi yangu.|

Sambaza....