Sambaza....

Baada ya klabu ya soka ya Simba kufanikiwa kuingia katika fainali ya michuano ya Sportpesa Supercup mchezaji wa zamani wa Everton ya England amewapotezea mabingwa hão wa VPL.

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria “The Super Eagle” na mshambuliaji wa zamani wa Everton ya England  alikuwepo katika mchezo wa nusu fainali uliowapeleka Simba katika fainali ya michuano hiyo kwa mikwaju ya penati.

Yakubu Ayingbeni akiwa na makocha wa timu ya Academy ya Everton walipewa jukumu la kuchagua nyota wa mchezo huo wa nusu fainali uliowakutanisha Kakamega Homeboys ya Kenya na Simba ya Tanzania.

Licha ya Erasto Edward Nyoni kucheza vizuri eneo lá ulinzi lá SimbaSc na kufanikiwa kupata mkwaju wa penati aliopiga lakini bado haikutosha kumshawishi Yakubu kumchagua kua mchezaji bora wa mchezo.

Yakubu alieichezea Everton michezo 82 na kuifungia mabao 25 alimchagua Moses Chikati kua nyota wa mchezo huo. Chikati alizawadiwa mpira na dola za Kimarekani 500 kama zawadii ya mchezaji bora wa mchezo huo wa nusu fainali.

 

Sambaza....