Shirikisho Afrika

Yanga sc kuondoka leo

Sambaza....

Kikosi cha Yanga sc, kinaondoka leo majira ya saa 9:00 za alasiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga sc, inakwenda kuvaana na USM Alger ukiwa ni mchezo wa kwanza hatua ya makundi utakaopigwa Jumapili ya wiki hii.

Akizungumzia safari hiyo, Meneja wa timu hiyo Hafidhi Saleh amesema kikosi chao kipo tayari na maandalizi yamekamilika kwa ajili ya safari hiyo.

Aidha Saleh, amekanusha uvumi ulionea kuwa wachezaji wa timu hiyo wamegoma kufuatia madai ya stahiki zao pamoja na mishahara.

Mapema leo Asubuhi Meneja huyo amekanusha uwepo wa taarifa hizo huku akisistiza kuwa hawezi kuongelea kwa undani suala la wachezaji kugoma.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x