Sambaza....

Kikosi cha Azam FC, kilichosafiri hadi Ruvu mkoani Pwani kinataraji kushuka dimbani leo hii kuwakabili Ruvu shooting ya Pwani, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara

Katika mchezo huo, Azam FC wanahitaji alama tatu ili kuwashusha mabingwa watetezi Yanga sc kwa muda kunako msimamo wa ligi ambapo Azam wataizidi Yanga kwa michezo miwili

Kunako msimamo wa ligi hiyo mpaka sasa Azam FC wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 45, na endapo wakishinda hii leo watafikisha alama 48, na kuishusha Yanga hadi nafasi ya tatu wenye alama 47

Kikosi cha kipo Mlandizi Pwani, tayari kwa mchezo huo ambao ulikuwa uchezwe jana lakini ulihairihishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha

Mchezo huo ulihairishwa baada ya uwanja wa Mabatini kuja maji, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku ya jana ambapo sasa mchezo huo utapigwa leo hii majira saa 10:00 za Alasiri

Sambaza....