Ligi Kuu

Hizi hapa mechi kali zakumalizia Ligi!

Sambaza....

Leo pazia la Ligi Kuu ya NBC linafungwa kwa jumla ya michezo yote 8 kuchezwa kwa muda moja ili kuepuka ujanja ujanja wa kupanga matokeo ikibidi.

Michezo ya mwisho ambayo inachezwa Leo ni kama ifuatavyo;

1 Kagera Sugar Vs Polisi Tanzania.

2 Coastal Union Vs Geita Gold

3. Dodoma Jiji Vs KMC

4.Ruvu Shooting Vs Tanzania Prisons

5. Mbeya City Vs Namungo FC

6.Mbeya Kwanza Vs Simba SC

7.Azam FC Vs Biashara United

8. Yanga vs Mtibwa Sugar

Mshambuliaji wa Coastal Union Adam Uledi “Balle” akimuacha mchezaji wa Polisi Tanzania.

Ukiingalia kwa ufasaha michezo hii vita bado vipo maeneo mengi hasa kwenye kushuka, kucheza play off na kuwakilisha nchi kimataifa.

Katika mechi ya siku kwangu mimi ya kwanza ni kati ya Azam Fc na Biashara United itakayopigwa Chamanzi.

Game hii endapo Azam anashinda anapata uhakika wa uwakilishia wa kimataifa kwa kushika nafasi 3 maana yake yeye hata husika na kuangalia matokeo ya FA kati ya Yanga na Coastal.

Iddi Nado wa Azam Fc akimuacha chini mlinzi wa Biashara United Boniface Maganga.

Na pia Azam atakunja kitita cha milioni 300 kutoka kwa wadhamini na haki za matangazo ya Television.

Lakini ikiwa hivyo moja kwa moja Azam atakuwa amemshusha Biashara United mwenye alama 28 ambapo atakuwa anaungana na Mbeya kwanza waliotupa mkono wa kwaheri kwenye micheo ya raundi ya 28.

Kikosi cha Tanzania Prisons kikiwa mazoezini.

Michezo mwingine wenye ushinda wa tofauti ni ule wa Ruvu Shooting na Tanzania Prisons ambao unabeba hatma ya yule anayekwenda kucheza Play off na ikibidi moja kushuka, yaani Tanzania Prison ambaye kama akipoteza kule Biashara akamfunga Azam basi atakuwa ameshuka akiwa na point 29.

Binafsi hii ndiyo michezo mikubwa miwili ninayoiangalia kwa jicho la uoga kwa kuwa ina maamuzi na hatma ya timu.

Fiston Mayele akiwaacha walinzi wa Mtibwa Sugar

Mchezo wa Yanga na Mtibwa nao una ladha yake Wananchi wakitaka kumaliza bila kupoteza mchezo huku Mtibwa aliye ‘dhofli khali’ akitaka kutumia mchezo huu kujinusuru na kucheza play off endapo atashinda huku pamoja una mapambano yake yote jicho na sikio lake litakuwa Mabatini kwenye mchezo wa Ruvu na Tanzania Prisons.

Lakini pia kuna vita kule kwa wenyeji Wagosi wa Kaya ambapo waitaikaribisha Geita Gold Mkwakwani. Coastal wao wapo sehemu salama hawashuki wala hawapandi kupata uwakilishi wa Kimataifa lakini kwa upande wa Geita wao wanahitaji uwakilishi kimataifa na kama wakishinda na Azam Fc akifungwa wao watakwenda kombe la Shirikisho.

George Mpole.

Pia katika mchezo huo kuna vita ya ufungaji bora ambapo George Mpole atahitaji mafanikio yake binafsi. Mpole ana mabao 16 sawa na Fiston Mayele hivyo kufunga kwake magoli au goli leo kutamfanya awe kinara wa upachikaji mabao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.