Uhamisho

Kroose: Ningekua mchezaji wa Man United!

Sambaza....

Kiungo fundi wa Ujerumani Toni Kroose amefichua kua alikua amekaribia kabisa kujiunga na Manchester United lakini mambo yakageuka ghafla baada ya David Moyes kufutwa kwazi katika klabu hiyo.

Mpaka sasa Kroose anaitumikia Real Madrid chini ya Zinedine Zidane huku akiwa mchezaji alieshinda vikombe vyote kwa ngazi ya klabu na timu ya Taifa.

Toni Kroose ” David Moyes alikuwa amekuja kuniona na mkataba ulikuwa umefanyika lakini baadaye Moyes alifukuzwa kazi na Louis van Gaal akaingia, ambayo ilikuwa ngumu sana,”

Toni Kroose  anaamini  Luis Van Gal ndie aliekwamisha mpango wake wa kwenda United

“Louis (Van Gal) alitaka wakati wa kujenga mradi wake mwenyewe. Sikusikia chochote kutoka United kwa muda mfupi na kuanza kuwa na mashaka. Halafu Kombe la Dunia likaanza na Carlo Ancelotti akapiga simu. Na ndiyo ilikuwa hivyo.”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.