Tetesi

Man U na Man City zakimbiana, Barcelona waikomalia City

Sambaza....

Tumekulea habari mbalimbali zilizogonga vichwa vya habari katika magazeti makubwa Barani Ulaya

Kiungo wa Brighton Alex Mac Allister amekiri yupo tayari kuondoka Brighton siku zijazo lakini akitamani kuendelea kusalia Uingereza. Manchester City wameonyesha kuhitaji huduma ya kiungo huyo ambapo itawabidi kupambana na Liverpool pia.[goal.com]

Real Madrid inavutiwa na mshambuliaji Julian Alvarez wa Manchester City ambae amekosa muda wakucheza Etihad. Madrid wapo tayari kuingia sokoni dirisha lijalo ili wapate msaada kwa nyota wao Karim Benzema.[goal.com]

Benardo Silva.

Klabu ya Barcelona ipo tayari kuendelea kumfwatilia na kupata saini ya nyota Mreno Benardo Silva wa Manchester City. Barca walimkosa Silva dirisha la msimu uliopita lakimi bado hawajaka tamaa na inatajwa thamani yake ni €80 milioni. [Telegraph]

Mshambuliaji wa Ajax Mohamed Kudus yupo tayari kuungana tena na kocha Eric Ten Hag katika timu ya Manchester United. Mpaka sasa Kudus amefunga mabao 16 katika michezo 31. United wapo tayari kumnyakua nyota huyo katika usajili ujao ili kuendelea kuipa makali timu yao. [Football insider]

United pia inamfwatilia mshambuliaji wa AS Roma Paul Dybala ambae anakipengele chakuuzwa kwa kiasi cha €12 milioni. Athletico Madrid pia wameonyesha nia ya mshindi huyo wa kombe la Dunia [Fuchjes].

Mohamed Kudus.

Droo ya michezo kwa kombe la FA imefanywa jana huku mahasimu wawili wa Jiji la Manchester wakitenganishwa. Manchester United watacheza na Fulham, Manchester City watavaana na Burnley. Michezo mingine Brighton watavaana na Grimsby, Sheffield United dhidi ya Blackburn Rovers.

Ngolo Kante amesema yupo tayari kuendelea kusalia Chelsea na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu licha ya sintofahamu inayoendelea katika kilabu chake cha Chelsea. [Bbcsports].

 

 

 

Sambaza....