Ligi Kuu

Mechi zilizoipa Ubingwa Simba!

Sambaza....

Baada ya kipigo cha magoli mawili kwa sifuri walichokipata Yanga kutoka kwa Tanzania Prisons katika dimba la Sokoine jijini Mbeya ni rasmi sasa SimbaSc ndio mabingwa wa Tanzânia Bara.

Baada ya kuukosa ubingwa kwa takribani miaka mitano msimu huu wa 2017/2018 SimbaSc inafanikiwa kuutwaa ubingwa huo huku ikiwa na michezo mitatu mkononi.

Mechi Zilizoipa SimbaSc ubingwa:

Mpaka kufikika kubakisha michezo mitatu huku ikiwa tayari bingwa Simba imepambana na kucheza michezo yote bila kupoteza. Huku ikiwa na wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa! Zifuatazo ni mechi zilizoamua ubingwa wa Simba msimu huu!

Tanzania Prisons 0 vs SimbaSc 1!

Katika dimba la Sokoine Simba imekua ikipata tabu kupata matokeo. John Bocco aliipa SimbaSc uongozi kwa goli lake la jioni kabisa na kuifanya kunyakua alama zote tatu.

SimbaSc 4 vs Singida utd 0!

Baada ya kupanda katika VPL timu ya Singida utd ilisajili vizuri na kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindani katika ligi! Lakini ilikutana na Simba iliyokua inajua nini inataka na kupata kichapo cha mabao manne katika uwanja wa Taifa bila tabuu.

SimbaSc 1 vs Azamfc 0!

Azam waliingia uwanja wa Taifa na kukutana na mguu wa Emmanuel Okwi kama ilivyo ada aliwaadhibu kama alivyozitesa timu nyingine katika VPL! Ushindi huu ulikua na maana kubwa kwani ili uwe bingwa ni lazima uwafunge unaogombea não ubingwa.

Mtibwa Sugar 0 vs SimbaSc 1!

Emmanuel Okwi kwa mara nyingine anaipa ushindi Simba katika dimba lá Jamuhuri Morogoro na kuzidi kuwasogeza kwenye ubingwa. Moja ya mechi ambazo Simba hawatozisahau msimu huu ni pamoja na hii dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simbasc 1 YangaSc 0!

Kumfunga mpinzani wako mnaegombania ubingwa ni sawa na kupata point sita. Maanaa kwa ushindi ule Simba ilipata point 3 na pia kupunguza tatu kwa Yanga.

Erasto Nyoni aliibuka kusikojulikana na kuipa ushindi Simba baada ya John Bocco na Emmanuel Okwi kushindwa kufunga mabao.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x