Ndemla
Ligi KuuTetesiUhamisho

Ndemla atua Yanga.

Sambaza....

Kwa tetesi ambazo tovuti ya Kandanda imezipata ni kuwa kiungo Said Ndemla ametua katika klabu ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa katika klabu ya Simba, amekubaliana na Yanga kwa asilimia kubwa kwa ajili ya kuvaa jezi ya njano na kijani msimu ujao.

Said Ndemla aliondoka Tanzania kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka nje ya nchi. Majaribio ambayo mpaka sasa hivi hatujui matokeo yake.

Said Ndemla ataungana na Ibrahim Ajib ambaye ashawahi kutoka Simba na Kuja Yanga na waliwahi kucheza pamoja katika timu ya Simba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.