Cristiano Ronaldo
Tetesi

Ronaldo anarudi zake Madrid!

Sambaza....

Cristiano Ronaldo huenda akarejea katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid, kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa Southampton Jose Fonte ambae ni mchezaji mwenzake wa timu ya Taifa ya Ureno Jose Fonte.

Ripoti nchini Italia zimesema kwamba Juventus itakua tayari kumuacha Ronaldo ajiunge tena na Madrid kwa ada ya pauni milioni 50 ili kujaribu kupunguza mzigo wa kifedha kwenye klabu unaosababishwa na janga la virusi  vya corona.

Cristiano Ronaldo akiwa na jezi ya Real Madrid

Jose Fonte “Ni wazi kwamba anaipenda klabu yenyewe, ni moja ya klabu kubwa zaidi duniani, ikiwa sio kubwa kabisa. Amebakiza marafiki wengi pale, na yeye huacha mlango wazi, kwa hivyo sitoshangaa kama atarudi tena  Real Madrid.”

Christiano Ronaldo  mshindi mara tano wa Ballon d’Or alijiunga na Juventus msimu wa 2018/2019 kwa ada katika wa pauni 100m. Mpaka sasa Ronaldo ameifungia Juventus mabao 53 katika michezo 75.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.