Said Ndemla
Tetesi

Said Ndemla awa lulu, wababe wanataka kumrudisha mjini.

Sambaza....

Kiungo wa Mtbwa Sugar Said Hamis Ndemla ameonekana kuwa lulu kabla hata Ligi haijamalizika kutokana na kiwango bora anachokionyesha akiwa na Wakata miwa wa Morogoro.

Said Ndemla alijiunga na Mtibwa msimu huu akitokea Simba Sc baada ya aliyekua kocha wa wa Simba wakati huo Didier Gomes kumkataa na kumuona ziada katika kikosi chake.

Kwa mujibu wa watu wake wa karibu Said Ndemla amepokea ofa kutoka kwa klabu iliyopanda daraja DTB Fc wakitaka huduma ya kiungo huyo wa zamani wa Simba. 

Dtb Fc yenye makazi yake Jijini Dar es salaam imejihakikishia kucheza NBC Premier League msimu ujao na tayari wameanza harakata za kukiinarisha kikosi chao.

“DTB wameonyesha nia ya kumtaka Ndemla kweli na tayari wametangaza dau lao watakalotoa, lakini bado Said hajaamua maana bado ni mapema huenda likatokea dili kubwa zaidi ya hilo hata Simba pia anaweza kurudi,” alisema mtoa taarifa ambae hakutana kuandikwa jina lake.

Said Ndemla

Klaby yake ya zamani pia Simba huenda ikafikiria kumrudisha tena kundini kiungo huyo ambae walianza nae tangu Simba B huku akikaa klabuni hapo takribani miaka 10.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.