Ligi Kuu

Simba Sc yapokea tuzo nyingine zaidi.

Sambaza....

G’Chaa Oyee! Tunasheherekea na Timu Galacha ya Msimu wa Ligi Kuu Bara 2019/20.

Mtandao wetu wa kandanda.co.tz umekabidhi tunzo ya Galacha Oyee katika kipengele cha ‘Timu Galacha ya Msimu‘ kwenda kwa klabu ya Simba SC. Tuzo hii inakabidhiwa kwa mara ya kwanza kwa klabu baada ya utaratibu wa kusheherekea na timu pamoja na wachezaji wanaofanya vizuri katika msimu unaomalizika.

Tunzo ya Timu Galacha ya Msimu waliyopewa simba sc

Tunzo hii imekabidhiwa kwa niaba ya mtandao huu na Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima ya MGen (MGen Tanzania Insurance), Bwana Jackson Kindikwili.

Akipokea tunzo hii Mratibu wa Shughuli za Simba Abbas Ally ameshukuru na kuupongeza mtandao wetu kwa kutambua mchango wa klabu yao na kwa ubunifu wa tunzo hii. Katika makabidhiano hayo, alikuwepo pia Meneja wa Timu, Bwana Patrick Rweyemamu.

Abba Ally (Kushoto) Akihojwa na Tigana Lukinja (Aliyeshika Simu)

Ikumbukwe klabu hii ilitoa Galacha wa Mabao wa msimu uliopita, na tulimkabidhi zawadi yake. Pia mtandao wetu umekuwa ukitoa zawadi kila mwezi kwa wachezaji wanaofunga mabao mengi kwa mwezi husika.

Bwa. Jackson Kindikwili (Kulia), akimkabidhi Mratibu wa Simba SC, Bwa. Abbas Ally (Kushoto).

Klabu ya Simba ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo sasa, wakifanya vizuri katika kuongoza Ligi na Ufungaji wa mabao pia.

Abbas (Kushoto), Jackson Kindikwili (Katikati) na Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu (Kulia)

Simba ilipata pia matokeo mazuri katika msimu wa 2019/20 dhidi ya vilabu vitatu Yanga, Azam na Tanzania Prisons ambavyo kwa msimu mitatu timu hizi zimeshika nafasi nne za juu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.