Cleotus Chama akimuacha kiungo wa Yanga.
Ligi Kuu

Yanga kagoma kuwa City, tegemeo kwa Wajelajela!

Sambaza....

Hakuna namna walaa maarifa mengine tena katika VPL msimu Simba sc wanahitaji alama moja tu ili waweze kuandika historia nyingine katika soka huku wakibakiwa na michezo sita mkononi.

Baada ya Yanga kugoma kumpa kombe Mnyama akiwa hotelini kama alivyofanya Manchester City mbele ya Liverpool na kumchapa Ndanda kibabe Taifa sasa hakuna namna ni Wajelajela pekee wanaosubiriwa kuchelewesha sherehe za Mnyama amaa kuamua kua ngazi ya ubingwa kesho katika dimba la Sokoine na kuamua kujipa mualiko wa “Party” la ubingwa Msimbazi.

John Bocco

Baada ya nahodha John Bocco kuingoza Simba kumfunga Mbeya City mabao mawili kwa sifuri Sokoine ni wazi sasa wamewapa kazi askari Magereza kuamua hatma ya ubingwa katika msimu huu.

Simba wanaingia Sokoine kesho kuivaa Prisons wakingia katika migoko ya Kibingwa wakitafuta alama moja tu ili kutunukiwa ubingwa wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu Bara ama kuamua kurefusha safari ya ubingwa na kusubiri mpaka mchezo wa Ndanda katika dimba la Nang’wanda Sijaona mkoani Mtwara.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.