Pascal Wawa
Ligi Kuu

Dilunga ni ‘tishio’ pekee kwa Wawa na Jjuuko, atawaadhibu?

Sambaza....

SAID Dilunga amecheza michezo tisa ya ligi kuu Tanzania Bara msimu huu na kufanikiwa kufunga magoli manne. Kiungo huyo mshambulizi wa Ruvu Shooting anataraji kuongoza safu ya mashambulizi ya Shooting siku ya Jumapili hii wakati timu yake itakapowakabili mabingwa watetezi Simba SC katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

VS WAWA NA JJUUKO…..

Dilunga mdogo wa Hassan Dilunga anayechezea Simba anataraji kuongoza mashambulizi ya Shooting kutokana na majeraha yanayomuandama mshambulizi mwenzake Issa Kanduru. Shooting haina matokeo mazuri sana kwani katika michezo tisa wameshinda mara mbili tu na kutoa sare nne huku wakipoteza michezo miwili.

Wanaingia kuwakabili Simba wakiwa na hali kubwa kutokana na ushindi wa kuvutia Jumatano hii walipoichapa Singida United 3-0 katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani. Safu yao ya mashambulizi imekuwa ikikabiliwa na tatizo kubwa la ufungaji kwani kuelekea mchezo wao wa kumi wamefunga magoli saba tu- Dilunga akifunga manne.

Kuifunga Simba kwa kumtegemea mfungaji mmoja tu ni kazi kubwa na Dilunga sasa anapaswa kuhakikisha ana-watala walinzi pacha wa Simba, Serge Pachal Wawa raia wa Ivory Coastal na Mganda, Jjuuko Murshid ili kuiepesha na kipigo timu yake mbele ya mabingwa hao watetezi ambao waliwachapa 7-0 msimu uliopita.

Licha ya kwamba katika michezo miwili waliyocheza pamoja, Jjuuko na Wawa nao wanattakiwa kumtazama mchezaji huyo mjanja mwenye kuhamahama eneo la hatari na kasi ya kuvamia goli.

NI VITA YA UFUNGAJI PIA….

Emmanuel Okwi alifunga magoli manne pekee katika ushindi wa Simba 7-0 Shooting msimu uliopita na alikuja kutwaa tuzo ya ufungaji bora mwishoni mwa msimu baada ya kufunga magoli 20. Mshambulizi huyo wa Uganda alianza msimu kwa kusuasua lakini ameamka na kufunga magoli manne katika michezo mitatu iliyopita.

Okwi amefunga mara nne msimu huu sawa na mshambilizi mwenzake kikosini Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere na huku nahodha, John Bocco akiwa tayari amefunga magoli mawili bila shaka mchezo huu wa Jumapili utakuwa si vita tu ya alama tatu bali pia ni mbio za kusaka kiatu cha ufungaji bora wa ligi.

Katika mchezo huu wapo washambuliaji wanne waliofunga magoli 14 hadi sasa katika ligi hivyo kwa namna yoyote itakuwa mechi yenye magoli ya kutosha . hadi sasa katika orodha ya wafungaji bora katika ligi- Eliud Ambokile wa Mbeya City ndiye anaongoza akiwa na magoli saba akifuatiwa na Vitalis Mayanga wa Ndanda FC NA Habib Kyombo wa Singida United ambao kila mmoja amefunga magoli matano.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x