Mabingwa AfrikaShirikisho Afrika

Ghana wajitoa kushiriki michuano ya Afrika.

Sambaza....

Katika kikao cha kamati ya muda ya kusimamia soka la Ghana Pamoja na Vilabu vya Ligi Kuu na ligi Daraja la Kwanza kilichokaa Ijumaa hii kimeamua kuwa hawatashiriki katika michuano ya Afrika msimu ujao.

Kamati hiyo ilikutana na Viongozi wa vilabu hivyo Katika hotel ya Alisa na kuamua hilo ikimaanisha kwamba Hakuna klabu yoyote kutoka Ghana ambayo itashiriki Ligi klabu Bingwa Afrika na Shirikisho Barani Afrika.

Ikumbukwe kwamba soka la Ghana limeingia doa toka mwishoni mwa mwezi June baada ya uchunguzi wa mwandishi Anas Aremayaw Anas kuibua shutuma nzito za Rushwa zilizowahusisha Viongozi na waamuzi wa soka nchini Humo.

Toka kipindi hicho ligi ya Ghana ilisimama Medeama SC wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu, huku Ashanti wakiwa nafasi ya pili na Asante Kotoko wakiwa wanatafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Shirikisho Afrika.

Ghana sasa inaungana na nchi kama Comoros, Guinea Bissau, Reunion, Mauritius, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia kushiriki michuano hiyo mwakani.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x