during the Premier League match between Chelsea and Liverpool at Stamford Bridge on September 16, 2016 in London, England.
EPL

Jurgen Klop kuendeleza ubabe wake kwa Chelsea?

Sambaza....

Liverpool wanakwenda Stamford Bridge kuvaana na wenyeji wao Chelsea, katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL, Liverpool wanaonekana wapo kwenye kiwango bora kwa sasa, lakini hii leo watatakiwa kudhihirsha ubora wao pale darajani

Chelsea wanaikaribisha Liverpool baada ya kushindwa kutetea ubingwa wao wa ligi, ikiwa ni baada ya kuutwa msimu uliopita

Miamba hii inakutana ikiwa imetofautiana kwa alama 6, ambapo Liverpool wakiwa na alama 72, huku Chelsea wakiwa na alama 66

Huu utakuwa mchezo wa 6 kwa kocha Jurgen Klop kukutana na Chelsea katika EPL, rekodi zinaonesha hajawahi kupoteza dhidi ya Chelsea akiwanga mara 2 na kutoka sare katika michezo 3

Chelsea hawana rekodi nzuri msimu huu dhidi ya timu zilizo kunako nafasi 6 za juu, wakiwa wamecheza michezo 9 mpaka sasa na kufanikiwa kushinda michezo miwili tu

Chelsea wanaonekana wapo vizuri kwa sasa, hii ni kutokana na takwimu za michezo minne ya hivi karibuni katika mashindano yote walipata matokeo mazuri

Mo Salah

Katika michezo 6 ya hivi karibuni iliyowakutanisha Liverpool na Chelsea, Liverpool hawajapoteza mchezo hata mmoja pia miwili kati hiyo walifanikiwa kushinda pale kunako dimba la Stamford Bridge

Olivier Giroud amefunga mabao 4 katika mechi 4 alizoanzishwa dhidi ya Liverpool, lakini pia Mohammed Salah amefunga katika michezo 4 ya mwisho alipokutana Chelsea akiwa FC Basel na Liverpool

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x