Sambaza....

Joto la pambalo la Watani wa Jadi tayari limeshaanza kupanda huku tambo zikianza mapema. Simba watakua mwenyeji katika pambano lotakalopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa November 5, Jumapili jioni.

Kuelekea pambano hilo Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba ametangaza ratiba yao huku wakionyesha kuutaka mchezo huo wa mzunguko wakwanza wa Ligi kuu ya NBC.

Katika mchezo ambao Simba watakua mwenyeji wa Yanga Ahmed alisema  “Kikosi kitaingia kambini kesho(leo) Jumanne, kwa kawaida mechi za ndani huwa tunaingia siku tatu kabla ya mchezo lakini hii tunawahi. Tumeutolea macho mchezo huu kuhakikisha tunapata ushindi.”

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga akiwa sambamba na meneja wa timu Walter Harisson wamekua wakionekana katika baadhi ya mechi za Simba wakicheza na timu za Al Ahly na Ihefu kuelekea mchezo huo mgumu. Hili lilimfanya msemaji wa Simba kutokulinyamazia na kumualika kocha huyo mazoezini pia.

“Kocha wao ameshakuja kwenye mechi tatu hadi sasa na leo tunatangaza kumkaribisha kwenye mazoezi yetu yatakayofanyika Mo Simba Arena. Tunamualika rasmi aje siku yoyote anayotaka.”

“Sisi hatuna jambo dogo hivyo tutafanya hamasa, ni mchezo wetu, tutautangaza tutakavyo tunajua watu watakuja lakini lazima tuichangamshe. Tutakuwa na wiki ya mchakamchaka wa kuaga kwao aage atarudi Jumatatu ya Novemba 6, 2023.”

Sambaza....