Sambaza....

Uongozi wa Lipuli FC, ya mkoani Iringa umesema kuwa wamekamilisha maandalizi yao na wamejipanga kuvunja rekodi ya Simba sc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Mchezo huo, unaotaraji kupigwa kesho Lipuli itakuwa kunako uwanja wake wa nyumbani wa kumbukumbu ya Samora mjini Iringa kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo Simba sc.

Kuelekea katika mtanange huo, Hafsa habari wa Lipuli Clement Sanga ametanaibaisha kuwa wamejapanga kuvunja rekodi ya Simba ya kutofungwa tangu kuanza kwa msimu huu wa 2017/18 hivyo amewataka wajiandae na kichapo cha zaidi ya bao moja

Simba sc, itaingia kunako uwanja huo ikiwa ndio vinara wa ligi hiyo kwa alama 58, za michezo 23, ikiwazidi mahasimu wao katika soka la bongo Yanga sc kwa alama 11 lakini wakiwa na michezo miwili mkononi

Sambaza....