Sambaza....

Shirikisho la soka nchini ( TFF) limeziagiza vilabu vya Coastal Union na Yanga sc, kufanya uchaguzi ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na viongozi wao waliojiuzuru.

Kwa mujibu wa balua iliyotoka kwa kaimu Katibu mkuu wa Shirikisho hilo kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho hilo, Rovacatus Kuuli, imezitaka klabu hizo kufanya uchaguzi haraka ili kujaza nafasi zilizo wazi.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga sc, Yusuf Manji, alijiudhuru kuitumikia klabu hiyo akieleza kuwa anahitaji kupumzika.

Mbali na Yanga sc pamoja na Coastal Union, pia AFC Arusha imetakiwa kutekeleza agizo hilo la TFF.

Sambaza....