Sambaza....

Bodi ya ligi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limeusogeza mbele kwa siku moja mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Lipuli FC dhidi ya Simba SC kutoka Aprili 20 hadi 21, 2018

Taarifa iliyotolewa na Ofsa mtendaji mkuu wa bodi, Boniface Wambura Mgoyo, kwenda kwa vilabu vya Lipuli na Simba, Mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Msimamizi wa kituo cha Iringa, Kamisa wa mechi, Kamati ya waamuzi na Wadhamini inasema kuwa sababu ya kuusogeza mbele mchezo huo ni uwanja wa Samora kuwa shughuli zingine siku ya Aprili 20

Lipuli FC vs Simba SC

TPL

“Sababu za mabadiliko hayo ni wamiliki wa uwanja kuutumia kwa shughuli nyingine ya kijamii” ilifafanua taarifa ya bodi hiyo

Simba SC itakwenda kuivaa Lipuli, ikitoka kuifunga Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 mchezo uliopigwa jioni ya jana kunako uwanja wa taifa jijini Dar salaam

Ushindi ambao unaifanya Simba SC, ifikishe jumla ya alama 58, baada ya kushuka dimbani mara 23, na kuendelea kuchanua kileleni ikiwazidi mahasimu wao Yanga SC kwa alama 11, lakini Yanga SC wakiwa na michezo miwili mkononi

Sambaza....