Sambaza....

Kikosi cha Simba SC, kinataraji kuondoka kesho nchini kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya Sportpesa Super Cup iliyopangwa kuanza June 3 mwaka huu jijini Nairobi, Kenya

Kikosi hicho, kitaondoka majira ya saa 1:00 asubuhi kwa ndege ya Shirika la ndege la Kenya KQ kikiwa kamili kwa ajili ya kuwania taji hilo

Mabingwa hao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, wamedhamilia kupeleka kikosi kizima kwa lengo la kutoa changamoto kwa wapinzani wao na kuipa heshima michuano lakini ikiwezekana kubeba taji hilo

Simba SC, ilionekana kuchukulia kawaidia michuano hiyo ilipofanyia mwaka jana jijini Dar es salaam lakini mwaka huu wanaonekana kuweka umuhimu mkubwa huku wakiahidi kubeba taji hilo

Mbali na Simba, mahasimu wao katika soka la bongo Yanga SC, nao wanataraji kupanda ndege hiyo kesho kuelekea nchini humo tayari kwa michuano hiyo

Sambaza....