Jonas Mkude
Ligi Kuu

Simba sc yapata pigo

Sambaza....

Kiungo wa klabu ya Simba, Jonas Mkude huenda akakosekana uwanjani kwa takribani wiki moja baada ya kuumia kifundo cha mguu akiwa mazoezini

Mechi za Simba zilizobaki

TareheMwenyeji-MgeniUwanja

Klabu hiyo, imekuwa ikifanya mazoezi yake kunako uwanja wa Boko veterani jijini Dar es salaam, ikijianda na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Njombe mji FC unaotaraji kupigwa Aprili 3, 2018 kunako uwanja Sabasaba mjini Njombe

Image result for Jonas Mkude aumia

Taarifa ya daktari wa klabu hiyo Yasin Gembe, imesema kuwa Mkude anaweza kuwa nje kwa wiki moja na sio siku mbili kama ilivyoripitiwa hapo mwanzo

Kiungo huyo aliyeibukia kunako timu ya vijana ya Simba sc mwaka 2011, alipata majeraha hayo baada ya kugongana na kiungo mwenzake Mzamir Yasin

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x