Sambaza....

[su_audio url=”http://www.kandanda.co.tz/wp-content/uploads/2018/01/Audio-ya-Story-ya-Tambwe.mp3″ autoplay=”yes”]

Mke wa mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga sc Amis Tambwe, hapa namzungumzia Naiyan Mohammed lakini kule mtaani kwao anajulikana sana kama “Mama Tambwe nilipata nafasi ya kupiga naye story na yeye akusita kufunguka

Naiyan au Mama Tambwe anasema yeye na Tambwe walikutana Dar es salaam, na ndoa yao kwa sasa ina miaka miwili ambapo wamebahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Aimar mwenye umri wa mwaka mmoja sasa

Mama Tambwe yeye ni mshabiki wa Mbeya city, lakini kabla ya mumewe kuichezea Yanga alikuwa shabiki wa Simba ambapo kwa sasa yeye ni shabiki wa Yanga sc.

Imezoeleka sana katika maisha ya mwanadamu, hasa mtu anapokuwa star au maarufu huonekana kuwa na maisha fulani hivi ya juu lakini hali hiyo tofauti kwa Tambwe mshikaji anaishi maisha ya kawaida sana

Akimuelezea mumewe yani Tambwe anasema ni mtu wa tofauti sana ” maisha ya Tambwe kama humjui huwezi kujua kama ni mchezaji, ana maisha fulani yani ya kawaida sana” alisema Naiyan

Aidha pia alisema Tambwe hupenda timu anayoichezea, ambapo kwa sasa Tambwe anaichezea Yanga sc hivyo ukimuliza bila shaka atakwambia anaipenda Yanga

Mama Tambwe alizungumza mambo mengi, lakini kubwa anasema mumewe huwa anakosa amani pale timu yake ya Yanga inapokuwa imepoteza mchezo

Pengine nisimalize uhondo huu wa story za Mama Tambwe hapa nikupe nafasi ya kumsikiliza zaidi.

Stori iliwekwa humu Abdallah Saleh  

Sambaza....