Sambaza....

Ule usiku wa Ulaya uliokua unasubiriwa kwa hamu kwelikweli na mashabiki wa dunia nzima umerudi tena.

Ligi ya mabingwa Ulaya imerudi tena kwa moto wa hali ya juu kwa ufunguzi wa mechi kali na tamu ambazo zinakata kiu ya kusubiri kwa muda mrefu.

Baada ya Real Madrid chini ya kocha Zinedine Zidane kuchukua ubingwa huo mara tatu mfululizo kipute kinatarajia kuanza tena cha kutetea ubingwa wao kwa mara ya nne mfululizo chini ya kocha mpya Mhispania  Julen Lopetegui.

 Mechi Kali!

Miongoni mwa mechi kali zinazotarajia kufungua michuano hiyo ni pamoja na wana fainali wa mwaka jana, lakini pia mabingwa wa Europa na matajiri wa Ufaransa! Mechi za mwanzo zitakazochezwa Jumanne na Jumatano hii September 18 na 19 ni:

Liverpool vs PSG.

Real Madrid vs AS Roma.

Mónaco vs Athletico Madrid.

Ukiachana na mechi hizo kali lakini pia kwa wapenzi wa timu za Uingereza wana hamu ya kuona vilabu vyao vitaanzaje msimu huu mpya wa mwaka 2018/2019. Baadhi ya timu za Uingereza zitakazoanza kampeni zao wiki hii ni :

Young Boys vs Manchester United

Inter Milan vs Totenham Hotspur.

Manchester City vs Olympic Lyon.

Sambaza....