Ligi Kuu

Yanga SC, yaitumia salamu Azam FC

Sambaza....

Yanga SC, wameondoa rekodi ya kutopata ushindi katika michezo 9 iliyopita kufuatia kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliopigwa kunako uwanja wa taifa Dar es salaam

Bao pekee katika mchezo huo, lilifungwa na kiungo raia wa Zimbabwe Thaban Scara Kamusoko kwa njia ya faulo mnamo dakika ya 25, ya kipindi cha kwanza

Matokeo hayo, yanaifanya Yanga kufikisha alama 51, na kuendelea kusalia kunako nafasi ya tatu huku Azam FC, wakiwa nafasi pili wakiwa na alam 55

Kabla ya ushindi wa leo, Yanga ilikuwa imepoteza mechi nne mfululizo katika ligi ikiwa ni dhidi ya Simba, Prisons, Mwadui FC na Mtibwa sugar

Ratiba inaonesha mchezo unaofata kwa Yanga wataikaribisha Azam FC, kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, hivyo kwa matokeo ya leo yamekuwa kama salamu kuelekea katika mchezo huo na Wanarambaramba hao.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x