Hakuna mshambuliaji wa Coastal mwenye idadi hiyo ya mabao mpaka sasa kwenye VPL. Mchezaji mwenye mabao mengi wa Coastal mpaka sasa ni Ayoub Lyanga mwenye mabao saba.
Beki wa pembeni wa timu ya soka ya Mwadui ya mjini Shinyanga Miraji Makka amesema imembidi kusafiri na timu kuelekea jijini Dar es Salaam ili kupambana na kuisaidia timu hiyo kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao watakapocheza na KMC.
Baada ya kuiondosha kwa mabao mawili kwa sifuri African Lyon katika uwanja wa Jenerali Isamuhyo Mbweni sasa KMC inasubiri mshindi kati ya Kagera Sugar ama Azam f c ili kucheza nae nusu fainali.