Sambaza....

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga sc, wanaendelea na maandalizi yao ya mchezo dhidi ya mahasimu wao katika soka la Tanzania Simba sc utakaofanyika Jumapili ya Aprili 29, 2018 kunako uwanja mkuu wa taifa

Taarifa kutoka Morogoro ambapo kikosi cha timu hiyo kimeweka kambi, zinasema kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi Andrew Vicent Chikupe “Dante” na Ibrahim Ajib Migomba afya zao zinaendelea kuimarika kufuatia kufanya mazoezi na kikosi hicho kwa takribani siku mbili

Pamoja na hao, pia mshambuliaji Donald Ngoma ameungana na kikosi hicho akijiandaa na mchezo huo unaovuta hisia za wapenzi wengi wa mchezo wa soka

Ngoma amekosekana uwanjani kwa muda mlefu, kutokana na kuuguza majeraha yake ya goti aliyopata katika mchezo wa ligi kuu mzunguko wa kwanza dhdi ya Mtibwa sugar

Pamoja na hao, pia mshambuliaji Amis Tambwe ameungana na kambi ya Yanga kuijindaa na derby hiyo inayotajwa kuwa ni ya tatu kwa derby zenye mvuto Afrika

Cairo derby inayozikutanisha Al Ahly dhidi ya Zamalek yenyewe inashika nafasi kwanza, huku ya pili ni kati  ya Kaizer chief dhidi ya Orlando Pirates huku mashemeji derby Gor Mahia dhidi FC Leopards ikishika nafasi ya nne

Sambaza....