Sambaza....

Beki wa kutumainiwa wa mabingwa wa zamani wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga SC, Kelvin Patrick Yondan, amemalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kusaini mkataba hii leo

Yondan, amemaliza tetesi iliyoenea kwa takribani wiki mbili kuhusiana na yeye kuondoka kunako klabu hiyo huku akihusiswa kujiunga na Azam FC

Akiongea na mwandishi wa tovuti hii ofisa wa klabu, alithibitisha kuwa Yondan amesaini mkataba wa miaka miwili mapema hii leo.

“Ni kweli Yondan tumemalizana naye kwa kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili leo na hivi sasa anelekea Nairobi kuungana na wenzake”

Beki huyo alijiunga na Yanga mwaka 2012 na kufanikiwa kuwa mhimili kwenye safu ya ulinzi ya klabu hiyo huku akisaidia kushinda mataji kadhaa

Pamoja na Yondan, Kifukwe aliisema kuwa Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera anatarajia kujiunga na kikosi jijini Nairobi hii leo akitokea Kongo DRC alipokwenda kwa majukumu ya timu ya taifa ya Kongo

Sambaza....