Blog

Tunashukuru sana kwa kutufikisha miaka 8

Sambaza kwa marafiki....

Leo tarehe 1 mwezi wa tano mwaka 2019 tovuti yetu ya kandanda.co.tz inatimiza miaka 8 tangu ianze rasmi kuandika habari za mpira wa miguu. Kwa kipindi hiki chote tovuti imefanya kazi na watu na makampunni mbalimbali kwa namna tofauti.

Uongozi wa kampuni ya GALACHA ambao ndio wamiliki na wasimamizi wa tovuti hii unapenda kutoa shukrani za pekee kwa wote walioisaidia tovuti hii kuendelea kuwepo na kubaki na lengo kuu la kutoa habari za mpira wa miguu pekee. Salamu hizi pia zifike kwa Mkurugenzi wa kampuni ya uuzwaji matairi, Binslum, Bwana Nassor Binslum kwa msaada wake wa mawazo na kutusaidia katika bonanza letu la kila mwaka la Kandanda Day.

Tovuti bado inabaki na vision ile ile ya kuwa sehemu maalumu ya uchambuzi, makala na takwimu sahihi bila kusahau habari zenye uweledi.

Salamu zetu zinanza kwa waandishi na wasimamizi wote ambao wanaandika sasa kwa kazi yao nzuri na kiumakini zaidi.

Mpiga picha/Mchambuzi: Sekwao Mwenda
Msimamizi Thomas Mselemu
Mchambuzi: Abdallah Saleh*
Mchambuzi: Martin Kiyumbi
Mchambuzi: Issack John
Mchambuzi: Baraka Mbolembole*

Wadau wote katika tasnia ya mpira wa miguu pia tunatanguliza shukrani zetu, hii ni kuanzia kwa viongozi wa Shirikisho, Vyama na Vilabu (Wasemaji na mameneja), Makocha na Wachezaji,  Vyombo vya Habari (Radio, Magazeti na Tv) na bila kuwasahau mashabiki wetu ambao siku zote wanatoa maoni yao ambayo yanatujenga pia.

Pia shukrani za kipekee ziawaendee  marafiki zetu hawa ambao kwa vipindi tofauti toka 2011 wameichangia tovuti kwa Makala,Uchambuzi au Habari

Dizo Moja(Assistant Lecture, Chuo Kikuu Zanzibar), Mussa Mwakisu (Mtangazaji EFM), Oscar Oscar JR (Mtangazaji EFM), Abdul Mkeyenge (Mwandishi Rai mwema), Damas, Clifford Ndimbo (Afisa Habari TFF), Paulo Manjale, Abdallah Saleh Jemedari (Mtangazaji Times FM), Jacky Maendaenda (GePG), Clevery Johnson, Rush (NMB), Allen Kaijage (Architect), Mohammed Mkangara (TFF, ofisi ya katibu mkuu), Maneno Hamis (Mwanafunzi wa DIT)


Kwa upande wa Graphics
Godblec Laiser na Samson wamewahi tusaidia katika vipindi tofauti


Tovuti imewahi kuwa na sehemu ya Katuni kutoka kwa:
Chris Katembo, Fede (Kiraka) na Said Michael


Picha zetu pia tumezitumia kwa makubaliano yasiyo rasmi na Michuzi Media Group

Othman Michuzi na Ahmad Michuzi


Kwa vipindi tofauti pia tumekuwa tukitumia Makala, Habari na Picha kutoka kwa watu binafsi au mitandao tofauti, kwa uchache tu tunaweza kusema asante kupitia kwa:
Shaffih Dauda, Edo Kumwembe, Samwel Samwel, Baraka Mpenja na Nicasius Nicholaus Agwanda

Tunashukuru sana kwa kutufikisha hapa tulipo, na safari inaendelea. Endeleeni kusoma makala, habari, uchambuzi na takwimu katika tovuti yetu. Pale panapohitajika tunapokea maoni na ushauri kwa mikono miwili.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.