Mabingwa Afrika

Mashabiki Yanga mmesikia maneno ya Mkwasa?

Sambaza....

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga sc, kesho watashuka kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuwakaribisha Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa raundi ya kwanza ya ligi ya vilabu bingwa barani Afrika

Kuelekea katika mchezo huo, Katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa “Master” amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwaongezea hamasa wachezaji

“Shabiki ni mchezaji wa 12, hivyo nawaomba wajitokeze kwa wingi kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu na hali ya kupambana zaidi” alisema Mkwasa

Pia katibu huyo, alisema kuwa kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, na baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea kwenye kikosi

“Yohana Mkomola, Abdallah Shaibu wanaungana na Obrey Chirwa pamoja naye Thaban Kamusoko kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho”

Mchezo huo unataraji kuchezwa kesho Jumanne, kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salamm, majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x