Stori

Mazembe Mpya Itafanikiwa!?

Sambaza....

Tout Puissant Mazembe lakini mitaa tunawafahamu kama TP Mazembe hawa ni mabingwa mara 11 wa michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu kuanzia Champions League, Confederation Cup mpaka Super Cup.

Pichani ni Moïse Katumbi Chapwe (juu) ambaye ni mfanyabiashara na mwanasiasa mkubwa sana pale DR Congo! Mzaliwa huyu wa Decemba 28 Mwaka 1964 amewahi kuwa Gavana wa Katanga Province ambayo ipo kusini mwa nchi ya DR Congo.

 

Katumbi alikuwa Gavana wa eneo hilo kuanzia mwaka 2007 mpaka 2015! Huku akiwa mwanachama wa chama cha People’s Party of Reconstruction and Democracy (PPRD) mpaka mwaka huo 2015.

Kabla ya kuzungumza zaidi kuhusu Moïse Katumbi Chapwe na soka kupitia TP Mazembe basi naomba ufahamu tu kwamba huyu ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa katika nchi hiyo na hata nje ya nchi au Bara la Afrika.

Miaka ya hivi karibuni Moïse Katumbi alipitia wakati mgumu kwenye masuala ya kibiashara baada ya kuwekewa vizuizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujihusisha kwenye masuala ya siasa hali iliyofanya klabu kushuka sana kiushindani hasa michuano ya vilabu ya CAF.

TP Mazembe inayoaukwa upya.

Baada ya anguko lao miaka ya hivi karibuni naona msimu huu wamerejea tena na wanataka kuonyesha ukubwa waliokuwa nao hapo nyuma! Kuanzia benchi la ufundi mpaka usajili wa wachezaji wapya umeongeza kitu ndani ya timu

TP Mazembe wamemrudisha Lamine Ndiaye kama kocha mkuu wa klabu hiyo ambaye pia amewahi kufundisha hapo mwaka 2010 hadi 2013 ambapo aliwapa ubingwa wa Afrika (CAF CL na Super Cup).

Vizuri! Kabla ya Lamine Ndiaye kurudi kocha mkuu alikuwa ni Pamphile Mihayo Kazembe ambaye pia alifundisha hapo 2017 hadi 2021 na aliwapa ubingwa wa Afrika! Kwa sasa Mihayo ni kocha msaidizi chini ya Ndiaye.

Benchi jipya la ufundi la TP Mazembe.

Wamefanya usajili wa wachezaji wazuri na wenye umri mdogo kama Cheick Fofana, Faisal Saaka, Ibrahima Keita, Mor Talla Mbaye, Boubacar Hainikoye, Aliou Faty, Jean Louis Diouf, Louis Ameka, Amadou Zon na mzoefu Rabih Ataya

Msimu huu wameanza vizuri Ligi kuu mechi 5 wakishinda 4 na sare 1 huku wakiingia Group Stage ya CAF Champions League. TP Mazembe wana CAF CL 5, Super Cup 3 na CAF CC 2!. Naona msimu huu wameamua kurudi kushindana tena.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

2 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote

Mimi ni shabiki wa TP Mazembe hasa pale inapokuja Dar kucheza na Simba (Mikia) KIPIGO CHA MWISHO alikula 3-2 Taifa

Ingawa TP wamekuwa kama Mbeya City tu siku za hivi karibuni.

2
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x