Gaston Sirino
Stori

Sirino: Wasauzi Walivyoiua Ndoto Yake ya Kucheza Kombe la Dunia

Sambaza....

Miongoni mwa vitu ambavyo vinamuumiza sana Gaston Sirino hadi leo ni Mamelodi Sundowns kuzuia uhamisho wake wa kuelekea Al Ahly.

Sirino kuanzia mwaka 2020 alihitaji kuondoka Mamelodi Sundowns na kuelekea Al Ahly hasa baada ya Pitso Mosimane kujiunga na Ahly kama kocha mkuu.

Hii ni miongoni mwa nukuu za Gaston Sirino ambazo amewahi kuzungumza kuhusu Al Ahly.

Mamelody Sundows “Masandawana”

“Natumai Mamelodi Sundowns itakubali ofa ya Al Ahly kwa ajili yangu. Al Ahly ni timu bora zaidi barani Afrika na ni ndoto ya kila mchezaji kucheza huko”.

May 22 Mwaka 2021 kwenye mchezo ambao walikutana Al Ahly dhidi ya Mamelodi Sundowns kwenye michuano ya CAF CL, Sirino alibadilishana jezi na Mchezaji wa Ahly ambahye ni Mohamed Afsha.

Baada ya tukio hilo, June 26 Mwaka 2021 Gaston Sirino aliposti picha ambayo walipigwa akiwa anabadilishana jezi na Mohamed Afsha kwa lengo la kuwatakia mchezo mwema Al Ahly ambao walikuwa wanaenda kucheza dhidi ya Esperance kwenye CAF CL.

Gaston Sirino na Pitso Mosimane.

Pitso Mosimane ambaye amewahi kuwa kocha mkuu wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly kwa nyakati tofauti kupitia South Africa FM Radio aliwahi kusema hivi.

“Al Ahly SC itasajili mchezaji kutoka Afrika Kusini. Yeye si wa timu yangu yoyote ya awali. Yeye sio Lorch au Sirino lakini mchezaji atakuja”.

Gastón Sirino ni mzaliwa wa Montevideo, Uruguay  mwenye umri wa Miaka 32 alizaliwa February 22 Mwaka 1991 na alijiunga na Mamelodi Januari 17, 2018 akitokea Bolívar La Paz ya Bolivia.

Gaston Sirino.

Mwaka 2019 June 26 thamani yake ndio iliongezeka na kuwa kubwa zaidi baada ya kufika €850k baada ya hapo alishuka na sasa thamani yake ni €350k(Kwa mujibu wa Transfer Market).

Majeraha ya mara kwa mara na kuugua ugonjwa wa Uviko 19 ilipelekea kwa kiasi kikubwa sana kupungua kwa ubora wa Gastón Sirino ambaye mkataba wake na Masandawana unamalizika June 30, 2028.

Sirino kama angejiunga na Al Ahly hapo nyuma basi angebeba ubingwa wa CAF Champions League na kucheza FIFA Club World Cup akiwa na Al Ahly.

Percy Tau.

Dirisha la usajili lililopita aliulizia kuondoka Mamelodi lakini ulikuwa ni wakati ambao Al Ahly hawahitaji tena huduma yake sababu wana Percy Tau kwa sasa.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x