Sambaza....

Baada ya ukanda wa CECAFA (Afrika mashariki) – (Tanzania, Kenya na Uganda) kushinda zabuni ya kuandaa mashindano ya makubwa zaidi kwa ngazi ya mataifa AFCON ya 2027, miji teule imeteuliwa ambayo itahusika na michezo itapigwa huko. KANDANDA.CO.TZ imeingia chimbo na imekuletea takwimu za idadi ya watu kwa kila nchi mwenyeji na idadi ya watu katika eneo husika.

Ni ukweli kwamba idadi kubwa ya watu katika eneo fulani hufanya mahitaji kuwa makubwa, idadi ya watu ndio huamua kiasi cha huduma ama bidhaa. Kwa Kenya mji teuliwa ni Nairobi na Mombasa, Uganda mji mwenyeji utakuwa Kampala na kwa upande wa Tanzania miji teuliwa ni Dar es salaam, pamoja na Arusha.

Miji hii yote katika nchi wenyeji inasifika kuwa na idadi kubwa pamoja na harakati nyingi za watu; na hizi ndio takwimu za watu katika miji hiyo.

TANZANIA

Katika nchi ya Tanzania majiji ambayo michezo inatarajiwa kufanyika ni Dar es salaam na Arusha.

Jiji la Dar es salaam linasifika sana kuwa na idadi kubwa ya watu pengine ikikadiliwa kuwa kubwa zaidi kuliko jiji lolote lile katika ukanda wa CECAFA (Afrika Mashariki), jiji hili linapatikana katika pwani ya Tanzania upande wa mashariki. Kwa sasa jiji hilo lina idadi kubwa sana ya watu ikikadiliwa kufikia milioni 7,776,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.01% toka mwaka 2022. Mwaka 2022 idadi ya watu jijini Dar es salaam ilikuwa ni milioni 7,405,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.08% toka mwaka 2021. Na idadi ya watu wa Dar es salaam kwa mwaka 2021 ilikuwa ni milioni 7,047,00 ikiwa ni ongezeko la aslimia 5.15% toka mwaka 2020. (Takwimu hizi ni kulingana na Macrotrends).

Jiji la Arusha, ni moja ya majiji maarufu sana katika ukanda huu wa Afrika mashariki likisifika kwa utalii na idadi kubwa ya watu. Jiji hili linapatikana kaskazini mwa Tanzania likikadiliwa kuwa iadadi kubwa ya watu wanaokadiliwa kufikia milioni 1.7 huku wakazi waishio mjini wakifikia laki 740,442 Ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.08 toka 2022. Mwaka 2022 idadi ya watu Arusha ilikuwa ni 519,00 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.77% kutoka mwaka 2021. Mwaka 2021 ilikuwa ni laki 505,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.43 toka mwaka 2020.

KENYA

Kenya ikiwa moja ya nchi mwenyeji hapa imeteuliwa miji miwili ambayo ni Nairobi pamoja na Mombasa.

Nairobi ndio.mji mkuu wa Kenya ambao una idadi kubwa zaidi ya watu kuliko mji mwingine wowote nchini Kenya. Inakadiliwa kuwa na watu wnaofikia milioni 5,325,000 kwa mwaka 2023, mwaka 2022 ilikuwa ni milioni 5,119,000 huku mwaka 2021 ikiwa ni milioni 4,922,000.

Mji wa mombasa wenyewe unapatikana upande wa mashariki mwa Kenya ambao uko Pwani, unasifika kuwa na idadi kubwa sana ya watu wanaokadiliwa kufikia milioni 1,440,000.

UGANDA

Uganda kama nchi mwenyeji pia michezo kadhaa itapigwa huko katika jiji kubwa zaidi nchini humo ambalo ni jiji la Kampala ambao ndio mji mkuu wa nchi hiyo. Jiji hili linasifika kuwa na idadi kubwa sana ya watu likisifika kuwa na harakati nyingi.

Jiji hili linakadiliwa kuwa na watu milioni 3,846,102 kwa mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la alimia 5.32%. Mwaka 2022 ilikuwa 3,652,00 ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.24% toka mwaka 2021.


Kumbuka: Mpaka kufikia 2027 ambapo fainali hizo za AFCON zitachezwa kutakuwa na ongezeko kubwa la watu kwani wageni toka sehemu mbalimbali duniani watakuja kushuhudia fainali hizo. Miji yote ambayo fainali hizi zitapigwa zina idadi kubwa ya watu hivyo tutarajie mafuriko makubwa ya watu viwanjani na vitajaa sana. Usisahau kwa sasa soka katika ukanda wa Afrika mashariki linakuwa kwa kasi sana huku muamko na hamasa ya kwenda Uwanjani ni mkubwa sana.

JE unafikiri fainali ya AFCON Itapigwa katika mji gani ? Usiwaze KANDANDA.CO.TZ inakupa nafasi ya kutoa maoni yako hapo chini katika sehemu ya maoni pamoja na kupiga kura hapa chini. Hii TAKEU ndio hii? Usisahau kutufuata katika kurasa zetu za kijamii kwa jina la kandanda.co.tz 

[poll id=”12″]

KARIBU KWENYE ULIMWENGU WA KANDANDA.


Sambaza....