Sambaza....

African Football League wengi wanaifahamu kama Super League! Kwanini Simba? Kwanini mechi ya ufunguzi ni Benjamin Mkapa na Tanzania?

Rahisi! Hivi sasa Tanzania inaendelea kutengeneza picha kubwa na nzuri kuanzia ushiriki wa klabu zetu kwenye michuano ya kimataifa mpaka timu za Taifa za wanaume na wanawake.

 

FIFA na CAF hawajaona shida kuleta mechi ya ufunguzi kati ya Simba dhidi ya Al Ahly ndani ya Jiji la Dar Es Salaam sababu wanaelewa njia inayochongwa hivi sasa katika soka ndani ya Tanzania.

Ukweli ni kwamba raia wa Tanzania wengi kwa sasa mchezo pendwa kwao ni mpira wa miguu, wanaupenda haswa na mpira umewapenda! Tumeamua kulipokea soka na uwekezaji ni mkubwa huku sasa unalipa.

Miaka mitano ya hivi karibuni kuanzia 2018 mpaka leo hii 2023 Simba wamekuwa na muendelezo mzuri sana kwenye michuano ya kimataifa na alama yao imebaki huko! Kuanzia mashariki, kusini, magharibi na hata kaskazini wamepita kote na kuacha alama.

Mchezp wa Simba dhidi ya TP Mazembe katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Simba wamecheza sana hatua ya makundi na robo fainali wamecheza nyingi sana kwenye michuano ya CAF! Ukanda huu wa Afrika Mashariki naweza kusema kuwa kwa miaka hii mitano wamefanya vizuri kuliko timu nyingine.

Uwanja wa Benjamin Mkapa  ni miongoni mwa viwanja vikubwa na bora sana Barani Afrika ndio maana FIFA na CAF wameona sio shida wao kuleta mechi hapa sababu kuna mechi kubwa pia zilishachezwa hapa hata kabla ya maboresho ya hivi sasa.

Kuanzia Fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika msimu uliopita, robo fainali ya Simba dhidi ya Al Ahly, TP Mazembe, Orlando Pirates, Kaizer Chief mechi nyingine kubwa za mashindano ya CAF hivyo hii sio kitu kigeni kwa Tanzania kuandaa mechi kubwa kama hizi.

Kibu Denis akipiga shuti mbele ya walinzi wa Orlando Pirates katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Vizuri! Hii ni fursa nyingine ya Tanzania kutangaza biashara ya mpira kwenda Duniani kwa ujumla! Sababu kuna ugeni mkubwa wa Rais wa FIFA Gian Infantino, Rais wa CAF Patrice Motsepe na viongozi wakubwa wa Mashirikisho mengine ya soka Afrika.

Super League ni mashindano mapya ambayo yanazindulia Afrika kwa mara ya kwanza sababu hata Mabara mengine bado hawajazindua hivyo hichi ni kama kipimo cha mpango huu wa FIFA katika soka la Dunia.

 

Sambaza....