Sambaza....

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga raia wa Ghana Hafidhi Konkoni amefunguka wazi kuwa anahisi presha kubwa katika klabu ya Yanga kutokana na kutopata nafasi ya kutosha kucheza.

Kuhamia Yanga kwa Konkoni kumekuja baada ya kuwa na msimu wa kipekee akiwa na Bechem United ya Ligi Kuu ya Ghana, ambapo alifunga mabao 15 na kushika nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora wa ligi hiyo.

Yanga walimsajili mshambuliaji huyo wa Ghana kuziba pengo la mshambuliaji wao bora, Fiston Kalala Mayele aliyejiunga na klabu ya Pyramids ya Misri. Katika mahojiano na Bryt FM ya Koforidua, Konkoni alikiri matarajio makubwa na uzito wa kuchukua nafasi ya fowadi huyo wa Kongo.

“Jukumu pekee la mshambuliaji ni kufunga mabao, ukweli ni kwamba nina presha ya kufanya kwa sababu niliingia kuchukua nafasi ya mshambuliaji mahiri Mayele ambaye ameondoka na kujiunga na Pyramids,” Konkoni aliuambia mtandano wa Ghanasoccernet na kuongezea;

“Mayele aliifungia Yanga mabao mengi. kabla ya kuondoka kwake, na ndivyo wanavyotarajia kutoka kwangu. Lengo langu ni kuifungia Yanga mabao mengi ifikapo mwisho wa msimu huu na pia kufikia malengo yetu,” Konkoni alisema.

Hafiz Konkoni

Tayari Hafiz Konkoni ameshaifungia Yanga mabao mawili tangu ahamie kutoka Bechem United wakati wa usajili wa hivi karibuni. Matarajio yake ni kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga huku wakijitahidi kutimiza malengo yao ya msimu huu.

Mshambuliaji huyo atakua na kibarua cha kurudi nchini kwao Ghana ambapo Yanga watakua na kibarua cha kuvaana na Medeama Fc ya huko katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sambaza....