Sambaza....

Mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Althur, amevunja mkataba wake na klabu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam baada ya kuitumikia kwa nusu msimu tu

Althur ambaye Ghana alikuwa akiitumikia klabu ya Liberty Professionals, amevunja mkataba na timu hiyo ya Dar es salaam kwa kile kilichoelezwa kutopewa muda wa kutosha wa kucheza

Licha ya kuwa na mwanzo mzuri kunako ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akianza kufunga bao katika mechi yake ya kwanza, Mghana huyo alitofautiana na kocha Aristica Cioaba ndipo alipoanza kumuweka benchi mshambuliaji huyo

Na baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Abdul Mohammed, ambaye ndiye aliyemsajiri na baadae kutimuliwa kwa Cioaba, Althur akapoteza kabisa matumaini ya kuitumikia klabu hiyo

Althur mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao sita katika michezo yake mitano ya mwanzoni na Azam FC kabla ya kuja kusugua benchi

Mshambuliaji huyo, alikuwa mfungaji tegemeo wa Liberty Professionals msimu uliopita kabla ya kujiunga na Azam FC, mnamo Januari mwaka huu akichukuwa nafasi ya Mghana mwenzake Yahaya Mohammed aliyevunjiwa mkataba

Sambaza....