Uhamisho

Huu ndio usajili bora VPL dirisha dogo?

Sambaza....

Ligi imesimama huku Simba sc ikiwa ndio kinara wa Ligi akiwa na alama 71 ikiwa imebaki mizunguko 10 ili Ligi kumalizika. Huku tayari kukiwa na migongano ya mawazo tofauti kuhusu kumaliza Ligi ama kusubiri mpaka hali ikae sawa na Ligi iendelee kama kawaida.

Katika dirisha dogo baadhi ya timu zilifanya usajili ili kuweza kujiimarisha katika Ligi, kuna timu zilizofaidika na usajili wao lakini wengine wakiwa bado hakieleweki. Tovuti yako ya Kandanda inakuletea sajili 5 bora mpaka sasa ligi ikiwa imesimama.

1. Benard Morrison – Orlando Pirates kwenda Yanga sc.

Winga Mghana aliesajiliwa na  Yanga kwa nguvu ya GSM akitokea Orlando Pirates. Moja ya sajili muhimu kabisa kwa Yanga msimu huu baada ya kuwapunguza Mastar wa kigeni  walisajiliwa dirisha kubwa wakionekana mzigo. Benard Morrison amekua akifanya mambo ya muhimu na yasiyo ya muhimu akiwa uwanjani. “Shibobo”, kasi, chenga na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao vimekua vikiwakosha mashabiki wa Yanga.

– Simba hawatomsahau kwa goli lake faulo katika mchezo wa March 8.

Benard Morison “shibobo style”

2. Luis Miquissone – UD Songo kwenda Simba sc.

Mwanzoni alikua aende Yanga baada ya kuwasha moto katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa akiwa na kikosi cha UD Songo katika mchezo dhidi ya Simba.  Baada ya kutua Simba yenye kikosi kipana haikuchukua muda sana kujitambulisha ni mchezaji wa aina gani, mwepesi akiwa na mpira na uwezo wa kuwapunguza mabeki wa timu pinzani ndivyo vitu vinavyoifanya Simba kuoenekana imelamba dume.

– Mchezo wa Simba dhidi ya Biashara United hakika alithibitisha ubora wake

Luis Miquissone alithibitiwa na wachezaji wa Yanga.

3. Never Tigere Fc Platinum kwenda Azam fc.

Mzimbabwe huyu isajiliwa kimyakimya bila mbwembwe nyingi akitokea Fc Platinum na mchezo wake wa kwanza ulikua dhidi  ya Yanga. Ni kiungo mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na kukaa na mpira. Kwa mwezi March tuu ameweza kufunga mabao matatu.

– Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa haswa karibu na eneo la hatari la mpinzani.

Never Tigere

4. Kevin Sabato Kongwe Gwambina kwenda Kagera Sugar.

Ilishangaza kidogo kwa yeye kuanza msimu akiwa na Gwambina ya daraja la kwanza lakini nusu msimu tuu ilitosha kumrudisha Ligi kuu. Kevi Kiduku ni yuleyule tuu mwenye kasi matumizi ya nguvu na uwezo mkubwa wa kupambana na mabeki. Kwa kujiunga na Kagera katika dirisha dogo mpaka sasa ana mabao 7 huku akiwa na hatrick moja dhidi ya Mwadui fc.

-Ameibuka Galacha wa mabao kwa mwezi February baada ya kufunga mabao matano.

Kevin Kongwe Sabato

5. Ditram Nchimbi – Polisi fc kwenda Yanga sc.

Baada ya kuwafunga  bao tatu akiwa na Polisi Tanzania na kuitwa timu ya Taifa Yanga wakaona isiwe tatu wakampa usajili na kuwakata kina Sidney  na Juma Balinya. Yanga wamekua wakifaidika na Nchimba akitokea  pembeni ama mshambuliaji wa kati kutokana na kasi yake na nguvu akiwa anashambulia lango la timu pinzani.

– Amefanikiwa kua mpishi mzuri wa mabao ya Molinga akitokea pembeni na pia ameweza kufunga mabao muhimu kwa Yanga akiwa kama mshambuliaji wa mwisho.

Ditram Nchimbi.

Tuambie ni kwako anafaaa kua usajili bora namba moja katika dirisha dogo na nina aliekuvutia kati ya sajili hizi tano, tupe maoni maoni yako.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.