Hazard akishangilia
La LigaTetesiUhamisho

Madrid yatenga zaidi shilingi bilioni 930 kuwanasa wachezaji hawa ….

Sambaza....

Kocha Mpya wa Los Blancos, Zinedine Zidane amedhihisha wazi kuwa nia yake ni kukisuka kikosi cha Madrid na kukipa thamani yake inayostahili na ushindindani unaotrajiwa na mashabiki kote duniani.

Kwa ushirikiano na Rais wa klabu hiyo Florentinop Perez, tayari wameshatenga Paundi millioni  300 zaidi ya  shilingi bilioni 930 za kitanzania kwa ajili ya usajili mpya  katika dirisha la usajili la kiangazi.

Wachezaji wanaowaniwa na kocha huyo kwa udi na uvumba ni mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji, Edin Hazard, mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza , Harry Kane, Raheem Sterling wa Man City na Sadio Mane wa Liverpool.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.