Uhamisho

Arda Turan kutimkia Uturuki

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona ya Hispania anakaribia kujiunga na klabu ya Istanbul Basaksehir ya nchini Uturuki

Istanbul Basaksehir inayoongoza kunako ligi kuu ya soka Uturuki wakiwa na alama 36, baada ya kushuka dimbani mara 17, wakipishana kwa alama moja na Garatasaray walio katika nafasi ya pili na alama zao 35, wakiwa wameshuka dimbani mara  17

Turan tangu ajiunge na Barcelona mwaka 2015  kwa kitita cha euro milioni 34, akitokea kunako klabu ya Atretico Madrid amekuwa akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku akiwa amefunga jumla  ya mabao 19, katika michezo 53, ya michuano yote

Arda Turan mwenye umri wa miaka 30, hajakichezea kikosi cha Barcelona tangu kuanza kwa msimu huu kikiwa chini ya kocha Ernesto Varvede

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x