
Michuano ya Sportpesa imeanza kutimua vumbi leo mchana ambapo timu ya Mamlaka ya Bandari ya Kenya imefungua dimba dhidi ya Matajiri wa alizeti Singida united.
Katika mchezo huo uliopigwa saa nane mchana katika dimba la Taifa Bandari fc ya Kenya imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Singida united bao moja kwa sifuri.
Bao pekee la Bandari fc katika mchezo huo limefungwa na William Wadri katika dakika ya 67 kwa njia ya mkwaju wa penati. Bandari walilapata mkwaju huo wa penati baada ya mlinzi wa Singida United Boniface Maganga kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Kwa matokeo hayo yanaifanya timu ya Bandari f c kufika hatua ya nusu fainali na hivyo kusubiri mshindi kati ya Yanga au Kariobangi Sharks.
Unaweza soma hizi pia..
Idd Chuji, viwanja vitau-miss umaridadi wa miguu yako!
Katika Chuji mmoja ulikua unaweza kupata viungo watatu kwa maana ya kiungo wa ulinzi, kiungo mchezeshaji na kiungo mshambuliaji, jamaa soka alilijua na lenyewe likamjua.
Haruna Moshi “Boban” amerudi!
Haruna Moshi msimu uliopita alikua akiitumikia Yanga chini ya Mwalim Zahera kabla ya msimu kuisha na Yanga kuamua kuachana nae lakini sasa amerudi kivingine tena VPL.
Tujadili Mechi za Leo Ligi Kuu ya Vodacom
Ungana nasi kupiga stori kuhusu mechi zote za leo Ligi kuu ya Vodacom Tanzania hapa, ukiwa pamoja na waandishi na wachambuzi wa kandanda.
Sevilla ndani ya Bongo!
Sevilla walioletwa nchini ni Sportpesa wanakuja kucheza na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sports Club mchezo wa kirafiki wa kimataifa nchini.