Sambaza....

Kiungo wa Kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Shakthar Donetsk, Frederico Santos, ameonekana akiingia katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Manchester United kwa ajili ya kukamilisha usajili wake

Fred, anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya siku ya leo na kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji halali wa klabu ya Manchester United

Fred atajiunga na United kwa ada iliyotajwa ya Euro 52 milioni

Frederico Rodriguez De Paula Santos, mwenye umri wa miaka 25, ni kati ya wachezaji tegemeo kunako kikosi cha Shakhtar Donetsk akicheza jumla ya michezo 101 na kufunga mabao 10

Mchezaji huyo kwa muda mlefu amekuwa akiwindwa na Kocha wa Man United, Jose Mourinho, na kwa sasa mpango unaeleka kufanikiwa

Sambaza....