EPL

Maneno machafu ya mashabiki yamuudhi Samatta

Sambaza....

Mitandao ya kijamii ina nguvu sana, kile kinachoaandikwa katika kurasa hizo kiwe cha mmliki wa akaunti husika au maoni ya mtumiaji yeyote yanaweza kujenga au kubomoa. Tumeona pia  mara nyingi hata wanasiasa wakitumia sehemu hiyo hiyo kutoa matamko au kuhamasisha jambo.

Mwaka huu unaweza kuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa kwa soka la Tanzania, baada ya Mbwana Samatta kufanikiwa kuingia Uingereza na kacheza katiks Ligi maarufu duniani ya EPL. Ligi ambayo ustaraabu wake unaweza kukufanya upigwe faini hata kwa kutema mate ovyo. Na kwao kila kitu ni biashara na muhimu zaidi ni katika kuikuza ligi yake vile iwezekanavyo.

vilabu vyote vinafaidika kwa kila kitu kuwepo Ligi Kuu, mfano mzuri na wa uhakika.. Mbwana Samatta ilipotangazwa kuwa yupo mbioni kuingia Aston Villa hadi kurasa za Aston Villa za mitandao ya kijamii iliongezeka wafuatiliaji kutoka takribani elfu 560 hadi kufikia sasa elfu 670. Kwa asilimia kubwa wakiwa ni Watanzania ambao waliifuata akaunti hii.


Haina ubishi Aston Villa waligundua ongezeko hili, na Samatta akapewa mapokezi mazuri ya kimtandao kwa ukaribisho wa Lugha ya Kiswahili kabisa. Wachangiaji wakaonekana ni waongeaji wa  Kiswahili zaidi tena zaidi, wakimsapoti mtu wao ambaye walitamani kumuona pale.

Tunatofautiana jinsi ya kupeleka ujumbe, lakini kwa mtazamo wetu, ukiangalia maoni ya wasomaji wengi yanaweza kukuudhi kama ukiyasoma kwa lugha yetu na hata ukiyabadili kwa lugha ya Kiingereza, si mazuri ya kujenga, japo yapo mazuri pia.

Tujifunze jinsi ya kuonyesha hisia zetu katika mitandao hiyo, la sivyo tunaweza kuwa tunaharibu milango ya wachezaji wengine kutoka Tanzania. Samatta ameshatuomba sisi kama Watanzania kuacha lugha za matusi na kuwasema wachezaji wengine pia katika kurasa zao, kwakuwa inaweza tengeneza pia uadui kati yake na wachezaji pamoja na mashabiki wake wapya.

Muhimu ni kuuelewa mchezo na kutoa maoni kistaarabu ya kujenga

Sambaza....