Blog

Mwambusi, chaguo bora Ihefu.

Sambaza....

Nitumie nafasi hii kumpongeza Kocha Juma Mwambusi ambaye kwangu ni sawa na Mzazi wangu kabisa (Baba)

Nilipita mikononi mwake pale Tukuyu Stars’ Banyambala ‘ na ninajivunia kuwa moja wa wanafunzi wake wa kwanza kwenye Career yake.

Alikuja kama Kocha msaidizi wa Athuman Juma Kalomba ( R.I.P) akitoka kwenye masomo yake ya Coaching.

Ninachoweza kusema ataongeza kitu kwenye timu ya Ihefu na atashare uzoefu wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye soka.

Anapokea nafasi ya kwanza ya Roommate wangu pale Mtibwa Sugar Zuber Katwila Kocha kijana ambaye bado ana nafasi ya kujifuza kwa uzoefu wa Mwambusi.


Mr Mwambusi pia ni Instructor wa ndani ( TFF) hivyo ana mengi ya kuyashusha chini.

Niwaonavyo Ihefu ni timu yenye malengo makubwa ya kufanya jambo kwenye industrial hii.

Ushahidi wa moja kwa moja ni uwekezaji wa uwanja wakianzia eneo la kucheza Pitch baada ya kufungiwa uwanja wao wakati fulani wamerejea kivingine sana

Na usajili wa Bwana Mwambusi unadhihirisha kusudio liliopo la kufanya timu bora yenye mfano ikiwepo kuwakumbusha baadhi juu ya kumiliki uwanja wako mwenyewe


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.